Mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA yazinduliwa rasmi Manyara - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA yazinduliwa rasmi Manyara

Mashindano ya mwaka 2019 ya Copa Coca-Cola UMISSETA yamezinduliwa rasmi mkoani Manyara leo ikiendeleza juhudi za Kampuni ya Coca-Cola kuunga mkono michezo mashuleni hapa nchini.


Uzinduzi huo umefanyikia katika Uwanja wa Kwaraa wikiendi hii, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akisubiria kuvalishwa kitambaa cha Scarf mara baada ya kuwasili mkoani Manyara kwa ajili ya kuzindua mashindano ya mwaka 2019 ya Copa Coca-Cola UMISSETA.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa Serikali, maofisa michezo, walimu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Manyara.


Akizundua michezo hiyo mkoani Manyara, Waitara aliishukuru Coca-Cola kwa kuwezesha michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA kuzinduliwa rasmi mkoani humo kwa mara ya kwanza huku akiwahimiza vijana wa Manyara kuthibitisha vi... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More