Mastercard na M-Pesa wazindua kadi inayowezesha kufanya manunuzi mtandaoni - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mastercard na M-Pesa wazindua kadi inayowezesha kufanya manunuzi mtandaoni


 Kwa mtu yeyote aliyewahi kufanya manunuzi ya kitu chochote bila kuinuka kitini ama kutoka nyumbani kwake anaweza kuelezea urahisi na wepesi wa kufanya manunuzi mtandaoni, lakini hii imekuwa ni ndoto kwa Watanzania walio wengi, mpaka sasa ambapo Mastercard wameungana na Vodacom na BancABC kutengeneza kadi ya kwanza itakayowezesha manunuzi mtandaoni – M-Pesa Virtual Card.

“Huduma ya M-Pesa kutoka Vodacom ina wateja Zaidi ya milioni 8.2 huku ikiwa na Zaidi ya wakala laki moja waliotapakaa nchi nzima, hii inawezsha upatikanaji wa uhakika wa huduma za kifedha, lakini imekuwa ni ngumu pale linapokuja suala la kulipia manunuzi mtandaoni haswa kupitia tovuti za kimataifa. Uzinduzi na ufanyaji kazi wa Virtual Card kupitia M-Pesa utaleta mapinduzi katika kuwezesha Watanzania kufanya manunuzi mtandaoni na kuondosha vikwazo ikiwamo kuwa na akaunti ya benki na pia hatari ya mteja kuweka taarifa zake za kibenki mtandaoni,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Hisham Hendi.

Inategemewa kwamba uunganisho wa intaneti kwa bara la Afrika itaongezeka sana ikiwa ni matokeo ya upatikanaji wa simu janja (Smartphone) na pia ukuaji wa utoaji huduma yenye kasi zaidi ya intaneti kutoka kwa watoa huduma kama Vodacom. Ongezeko hili la upatikanaji wa huduma ya intaneti litaongeza uhitaji wa maudhui ya kidijitali, mitandao ya kijamii, M-Commerce, elimu ya mtandaoni na pia malipo mtandaoni kurahisishwa na kuongezewa usalama zaidi.

Kadi hii itawawezesha wateja wa M-Pesa kufanya malipo ya aina yeyote kwa tovuti za kimataifa au za hapa nyumbani, ama kwa kutumia zana (App) yeyote ambayo inatumia na Mastercard kwa malipo, bila kuhitajika kuwa na akaunti ya benki au kadi ya mkopo (Credit Card). Wateja wanaweza kutengeneza virtual card kupitia menyu ya M-Pesa ama kupitia App yetu ya M-Pesa (huduma hii tutaiongeza hivi karibuni) na kuijaza pesa kupitia mfumo wetu wa M-Pesa. Kadi hii inakuwa tayari kwa matumizi mara tu baada ya kujazwa pesa.


Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (Kati), Raisi wa Kusini mwa Sahara wa Mastercard, Raghay Prasad (kushoto) na Mkuu wa hazina na kitengo cha soko la kimataifa wa Banki ABC, Barton Mwasamengo (kulia) wakionesha ushirikiano kati ya M-Pesa na Mastercard uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (Kati), Raisi wa Kusini mwa Sahara wa Mastercard, Raghay Prasad (kushoto) na Mkuu wa hazina na kitengo cha soko la kimataifa wa Banki ABC, Barton Mwasamengo (kulia) wakionesha ushirikiano kati ya M-Pesa na Mastercard uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Source: Issa MichuziRead More