MATAIFA ZAIDI YA 75 YASHIRIKI KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI, SERIKALI YATOA NENO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MATAIFA ZAIDI YA 75 YASHIRIKI KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI, SERIKALI YATOA NENO

Na Said Mwishehe,Globu ya jamiiSERIKALI imesema imejipanga vema kuhakikisha sekta ya nishati na hasa ya mafuta na gesi inawanufaisha Watanzania wote na kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano January Makamba wakati anafungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya mafuta na gesi wakati anamwakilisha mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya wadau 200 kutoka mataifa zaidi ya 75 duniani na moja ya ajenda ni kuangalia fursa ambazo zinaweza kupatikana katika sekta ya mafuta na gesi huku pia kongamano hilo likijita kuangalia fursa ambazo watanzania watanufaika nazo kutokana na uwepo wa miradi mikubwa inayoendelea nchini.
Hivyo Waziri Januari Makamba amesema ujumbe wa Waziri Mkuu katika kongamano hilo ni kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta ya gesi na mafuta.
"Pia Serikali imeweka m... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More