Matokeo ligi kuu Uingereza Man United yabanwa mbavu,City,Liverpool mambo safi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Matokeo ligi kuu Uingereza Man United yabanwa mbavu,City,Liverpool mambo safi

Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea kwa siku ya leo kwa kuchezwa michezo 7 huku mmoja ukitarajiwa kupigwa usiku huu kuanzia saa moja.Katika michezo hiyo timu kubwa zimeshuka uwanjani tatu ambazo ni Manchester United,Manchester City pamoja na Liverpool.Katika timu hizo kubwa Manchester United waimenyana na Wolverhampton huku majirani zao Manchester City wakisafiri umbali mrefu kwenda kumenyana na Cardiff City lakini majogoo Liverpool waliwakaribisha watakatifu Southampton.Katika michezo hiyo Man United amebanwa mbavu nyumbai kwao kwa kuazimishwa sare ya goli 1-1 na Wolves huku majirani za wakipata ushindi mnono wa goli 5-0 dhidi ya wenyeji wao Cardiff na Majogoo Liverpool wakiendelea kujikita kilelele kwa kufikisha alama 18 kibindoni wakicheza michezo 6 na kushinda yote.Mpaka sasa Manchester United amecheza michezeo 6 akishdinda michezo 3 akifungwa 2 na kusuhu 1 na anashikilia nafasi ya 6 akiwa na alama 10 mkononi.


na hayo ndio mastokeo yenyewe.By Ally Juma


The post Matokeo l... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More