MATUKIO MBALIMBALI YA DKT.MABODI SONGEA VIJIJINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MATUKIO MBALIMBALI YA DKT.MABODI SONGEA VIJIJINI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Songea Vijijini kuharakisha Uchunguzi wa Matumizi ya Fedha ya Shilingi Milioni 10 zinazosadikiwa kutumiwa vibaya katika Ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Kijiji Cha Mpangula Kata ya Matimila. 
Fedha hizo zilikuwa za kumalizia Matengenezo ya mwisho ya Kituo hicho kwa kupiga Plasta,Sakafu,milango na Jipsomu na zikaisha bila Jengo hilo kukamilika.   
Agizo hilo amelitoa katika mwendelezo wa ziara yake Mkoani humo katika Wilaya ya Songea Vijijini wakati akikagua Ujenzi wa Kituo hicho kilichojengwa kwa Michango ya Wananchi kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya  pamoja na Fedha za Mfuko wa  Jimbo la Peramiho chini ya Mbunge wake Mhe. Jenista Mhagama. 
Aliisisitiza TAKUKURU kukamilisha Uchunguzi huo kwa haraka ili kupisha shughuli zingine ziendelee kwa lengo la kukamilisha  Ujeni wa Kituo hicho na Wananchi wapate huduma za... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More