Maugo amchapa Mmalawi, Class amnyamazisha Mazola kwa TKO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Maugo amchapa Mmalawi, Class amnyamazisha Mazola kwa TKO

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo wa Tanzania amemchapa kwa pointi, mpinzani wake, Charles Misanjo wa Malawi katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Middleweight kwenye ukumbi wa PTA jijini. Wakati Maugo anashinda kwa pointi, bondia nyota nchini,Ibrahim Class alidhihirisha ubora wake baada ya kushinda kwa Technical knockout (TKO) raundi ya tano katika uzito wa Super Feather.
Pambano hayo yaliandaliwa kwa lengo la kutafuta mataulo ya kike kwa wanafunzi wa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa kushirikiana na taasisi ya She Can Foundation. Katika pambano hilo lililoandaliwa na promota wa kwanza wa kike nchini, Sophia Mwakagenda wa kampuni ya Lady In Red Promotion, Maugo alipata pointi 77-75 kutoka kwa jaji, Mwinyi Milla,  78-74 (Modesti Rashid) na 76-76 kutoka kwa jaji, Chaurembo Palasa.Bondia Mada Maugo (kulia) akirusha konde kwa Charles Misanjo wa Malawi katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Middle lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA juzi. Maugo alishinda ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More