Mawakala maji shingoni, ada za uhamisho kulipwa na wachezaji wao - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mawakala maji shingoni, ada za uhamisho kulipwa na wachezaji wao

Viongozi wa Ligi kuu ya soka ya Uingereza wanatarajiwa kukutana kesho alhamisi katika kuangalia jukumu la malipo kutoka vilabu kwenda kwa wachezaji.


Wachezaji wa Ligi kuu ya Uingereza huenda wakalazimika kuwalipa mawakala wao (ada ya usajili ya wakala ). Hapo awali vilabu husika vilikuwa na jukumu la kuwalipa mawakala.


Haya ni mageuzi ambayo yanatazamiwa kuwa makubwa katika soka la Uingereza.


Takwimu zinasemaje?


Kwa mfano vilabu vya Premier League msimu wa 2016 vililipa kiasi cha  £174m kwa mawakala, kutoka £130m, msimu wa 2015. Manchester City ndio timu iliyolipa mawakala (£26.3m) huku Chelsea wakilipa (£25.1m) na Manchester United (£19m) kwa msimu huo.


Je kuna madhara yeyote katika hili?


Huu mchakato utapelekea  wachezaji kuhitaji mishahara mikubwa.


Je upande wa vilabu nao watafaidika nini?


Kumekuwa na kasumba ya vilabu kuweka dau kubwa sana kwa wachezaji ili kukidhi haja na matakwa ya mawakala. Na wakati fulani kuna mawakala wamekuwa wakichochea vilabu husika kuweka bei kibwa... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More