MAZOEZI YA PAMOJA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAZOEZI YA PAMOJA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI


MAJESHI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yapo imara kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchi wanachama baada ya kuhitimisha mazoezi ya pamoja yaliyozikutanisha nchi hizo mkoani Tanga .

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi Dr Husein Mwinyi wakati wa kufunga mazoezi hayo ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi wanachama.

Aidha Dkt Mwinyi alisema kumekuwepo na ufanisi wa hali ya juu wa utayari wa kukabiliana na majanga kama hayo hivyo jukumu lipo kwa vikosi hivyo kujiamini na kutumia mbinu walizopata ili kuzisaidia nchi zao. “Tunaimani sasa baada ya mazoezi haya kwanza vikosi vyetu vitakuwa imara zaidi lakini ni wakati wa kuanza kupambana na matukio kama hayo si kwa nchi mojamoja bali kwa kushirikiana zaidi”Alisema Dr Mwinyi.

Mazoezi hayo yalizikutanisha nchi zote wanachama ikiwa pamoja na Tanzania ambae ni mwenyeji,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi huku Sudani kusini haikufika kutokana... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More