Mbao FC inaongoza ligi nini kipo nyuma ya pazia? - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbao FC inaongoza ligi nini kipo nyuma ya pazia?

Klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kwa ndio inaongoza ligi kwa sasa ikiwa na pointi saba (7) baada ya kucheza mechi tatu na kufanikiwa kushinda michezo miwili na kutoka suluhu mchezo mmoja.


Matokeo ya Mbao FC katika mechi tatu za kwanza za msimu huu kwenye ligi: Alliance 0-1 Mbao, Stand United 1-2 Mbao, Singida United 0-0 Mbao.


Mwenyekiti wa klabu hiyo Solly Njashi ameeleza kinachoifanya Mbao kufanikiwa katika mechi za kwanza za msimu huu.


“Ushirikiano wa wachezaji, viongozi na mashabiki pamoja na wadhamini nadhani ni vitu ambavyo vikiungana pamoja vinaleta ushindi hivyo naamini kama tutaendelea kushirikiana na umoja huu uliopo tutaweza kufanya vizuri.”


“Msimu huu tumebaki na wachezaji wengi, wapo walioondoka lakini waliobaki ni wengi. Nimejifunza kitu, wachezaji wengi wanapobaki baada ya dirisha la usajili wakiungana na wachache waliosajiliwa kuna kitu kinaongezeka.”


“Lakini kila mwalimu ana-falsafa yake hatuwezi kuzungumzia sana hilo lakini ndio safari imeanza tutaona huko m... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More