MBAO FC YAALIKWA KWENYE MICHUANO YA SPORTS PESA SUPER CUP - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBAO FC YAALIKWA KWENYE MICHUANO YA SPORTS PESA SUPER CUP

Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.

KLABU ya Mbao FC inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara imealikwa kwenye michuano ya Sports Pesa Super Cup inayotarajiwa kuanza Januari 22 mwaka 2019.
Ikiwa ni mara ya tatu ya michuano hiyo tangu ianzishwe hapa nchini ambayo inazikutanisha timu za Tanzania na Timu za Kenya zinazo dhaminiwa na Kampuni hiyo ya Kubashiri ( Sports Pesa)
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas amesema kuwa sababu ya kuialika Mbao FC kwenye michuano hiyo ni kutokana na Klabu hiyo kuonesha ushindani mkubwa kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.
Kwa upande wa uongozi wa Klabu ya Mbao FC kupitia kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Solly Zephania Njash amesema anaishukuru Kampuni ya Sports Pesa kwa kuialika timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano hiyo na wanaamini watafanya vizuri kwenye michuano hiyo.
"Naishukuru Sports Pesa kwa kutupa heshima hii ya kutualika katika michuano hiyo na mu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More