Mbao yamdondosha Salum Mayanga - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbao yamdondosha Salum Mayanga

Uongozi wa Mbao FC umefikia makubaliano na Salum Mayanga kuwa kocha wao mkuu kuchukua nafasi ya Ally Bushiri ‘Benitez’ ambaye amesitishiwa mkataba kutokana na mwendelezo wa matokeo mabovu ya klabu hiyo.


Inaelezwa kuwa, Mayanga amesaini mkataba wa kuifundisha mbao hadi mwisho wa msimu huu.


Kabla ya kutua katika ‘Wabishi’ Salum Mayanga alikuwa mkurugenzi wa ufundi wa Mtibwa Sugar huku pia akiwa amewahi kuwa kocha timu hiyo kwa mafanikio.


Mayanga amewahi kufundisha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kabla ya kocha wa sasa Emmanuel Amunike.


Source: Shaffih DaudaRead More