MBEYA CITY YAISHINDILIA RUVU SHOOTING 4-2, NDANDA YAIBWAGA MTIBWA NANGWANDA, AZAM FC SARE TENA ‘MIKOANI’ - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBEYA CITY YAISHINDILIA RUVU SHOOTING 4-2, NDANDA YAIBWAGA MTIBWA NANGWANDA, AZAM FC SARE TENA ‘MIKOANI’

Na Mwandishi Wetu, MBEYA
TIMU ya Mbeya City imefanya mauwaji katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Ruvu Shooting ya Pwani mabao 4-2 katika mchezo wa jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Eliud Ambokile alifunga mabao mawili ndani ya dakika tatu, ya 20 na 23 na Mbeya City ikaenda kupumzika inaongoza 2-0, kabla ya Khamis Mcha kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 52.
Iddi Suleiman ‘Nado’ akafunga dakika ya 60 na Peter Mapunda akaongeza lingine dakika ya 75 Mbeya City wakifikisha mabao manne, kabla ya Said Dilunga kuifungia tena Ruvu dakika ya 90.
Mechi nyingine ya leo, Ndanda FC imedhihirisha msimu huu imeimarika baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mbeya City imeichapa Ruvu Shooting ya Pwani 4-1 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo

Haukuwa ushindi mwepesi kwa wenyeji hao, kwani walilazimika kutoka nyuma kwa bao la mapema la mshambuliaji mwenye mwili mkubwa, Stahmili Mbonde dakika ya 23 ili... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More