MBINU ZITUMIKAZO KATIKA UKWEPAJI WA KODI ULIOKITHIRI TANZANIA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBINU ZITUMIKAZO KATIKA UKWEPAJI WA KODI ULIOKITHIRI TANZANIA

Baadhi ya kampuni au mashirika yanayofanya kazi hapa nchini (Tanzania) yana kampuni zake tanzu au mama nje ya nchi. Hili kimsingi halina ubaya. Ubaya unakuja pale ambapo kampuni hizo tanzu au kampuni mama; zinapotumika kufanya udanganyifu wa kukwepa kodi, tozo, malipo ya mrahaba pamoja na gawio. *Na udanganyifu huo mara nyingi hufanyika kwa kuongeza gharama za uendeshaji ili kupunguza kiwango cha faida ambacho kampuni zilizopo hapa nchini zinapata; ama zinaonekane zinapata hasara*. Ujanja huu kwa kitaalamu unaitwa *transfer pricing*.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo hayo, mbinu mojawapo inayotumika ni katika ununuzi wa mitambo na vipuri. Ili kupandisha gharama za uendeshaji, kampuni za hapa nchini huagiza vifaa hivyo kupitia kampuni tanzu au mama zilizopo nje ili Serikali isifahamu gharama halisi*. Kampuni hizo tanzu zikishanunua vifaa hivyo huviuza kwa kampuni za hapa nchini kwa bei ya juu; wakati mwingine mara tano zaidi ya bei halisi. Na kwa vile sheria zetu za kodi na uwekezaji zina... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More