MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAFANA, DC KIZIGO ATOA NENO LA SHUKRANI KWA WATANZANIA ,WANARIADHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAFANA, DC KIZIGO ATOA NENO LA SHUKRANI KWA WATANZANIA ,WANARIADHA

Na Ripota Wetu ,Globu ya jamii

WILAYA ya Namtumbo mkoani Ruvuma imefanya Mbio za Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon ambapo wanariadha mbalimbali akiwamo Godefrey Masaki wa JKT Arusha walishiriki.

Katika mbio hizo Masaki alishinda kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kushinda mbio za kilometa 21 huku akimuacha Mohemed Dule kutoka kikosi cha KG Songea aliyesgika nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Ostin Kinyunyu kutoka mkoani Njombe.

Pia kwa upande wa wanawake katika mbio hizo Magdalena Crispin kutoka Arusha ameibuka mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 21 huku mkimbiaji machachari Fabiola John kutoka Jeshi la Polisi Dar es Salaam akiibuka mshindi wa pili na kumwacha Adelina Irasias kutoka Dar es Salaam akishikilia nafasi ya tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo aliyeshiriki mbio za kilometa 2.5 akivalia nambari 021 amewashukuru Watanzania hasa wanariadha walioshiriki mbio hizo kwa kujitokeza k... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More