Mbona iko hivi: Jipangeni Fainali ni kwa ajili ya kushinda, sio kucheza! - Mwanaspoti | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbona iko hivi: Jipangeni Fainali ni kwa ajili ya kushinda, sio kucheza!

KWA yakini sikumbuki ni nani hasa aliyeibuka na kauli hiyo ambayo imetengeneza kichwa cha habari cha makala haya, lakini ni kauli ambayo makocha wa michezo yote hupenda kuwaambia wachezaji wao.
Katika mechi ya fainali ya mashindano ya aina yoyote, jambo la muhimu zaidi ni kutwaa kombe kwa sababu ndiyo kitu pekee kitakachobakia katika historia.
Jose Mourinho hubandika ujumbe huu ukutani kabla ya mechi yoyote ya kutwaa kombe. Falsafa hii tayari imefanya kazi kwake; amecheza fainali mbili za Kombe la Mabingwa wa Ulaya akiwa na timu mbili tofauti –Inter Milan ya Italia na Porto ya Ureno na ametwaa ubingwa mara zote hizo.
Kauli hii maarufu ilinijia mara baada ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Liverpool na Tottenham zote za England.  Majogoo wa Anfield walishinda 2-0 na kutwaa ubingwa; safari hii ikiwa mara yao ya sita kufanya hivyo.
Hata hivyo, haukuwa ubingwa rahisi kwa Liverpool hususani kwa washabiki wao. Mechi ilikuwa ngumu na Spurs kwa kweli walitawala mechi ile... Continue reading ->


Source: MwanaspotiRead More