MBOWE AAMUA KUTOA YA MOYONI KUONDOKA KWA LOWASSA CHADEMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBOWE AAMUA KUTOA YA MOYONI KUONDOKA KWA LOWASSA CHADEMA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
BAADA ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuamua kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema kwa kuwa ameondoka basi akawe mkweli huko alikokwenda. 
Lowassa wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliondoka CCM na kwenda Chadema ambapo wakati wa mapokezi yake Mbowe alisema amebadili gia angani. Hivi karibuni Lowassa alirejea CCM akisema amerudi nyumbani. Akizungumza leo Machi 16,2019 jijini Dar es Salaam Mbowe amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakimuuliza kuhusu msimamo wa Chadema baada ya Lowassa kuondoka. 
"Chama chochote cha siasa kina wajibu wa kujenga chama ikiwa pamoja na kuongeza wanachama na katika kuongeza huko wanachama tulimuongeza na mzee Lowasaa mwaka 2015.Nataka kulizungumza kwa kifupi sana, vyama vyetu vya siasa vinavuna watu mbalimbali, wapo wema, wapo wasio wema, wapo wanaopenda madaraka, wapo kila mmoja kwenye roho yake anajua anataka nini katika siasa, hapa mezani huenda tunaajen... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More