Mbowe Afunguka Makubwa Kuhusu Maisha ya Gerezani Yalivyoyakusikitisha - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbowe Afunguka Makubwa Kuhusu Maisha ya Gerezani YalivyoyakusikitishaMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Taifa, Freeman Mbowe amesema, amekutana na mambo ya kuumiza alipokuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, tangu Novemba 2018.


Akizungumza na wanahabari leo tarehe 15 Machi 2019 jijini Dar es Salaam, Mbowe ametaja changamoto zinazowakabili wafungwa katika gereza la Segerea huku akikazia kuhusu tatizo la wanaofungwa bila hatia.

“Kuna ugonjwa uliopo magereza kwa lugha ya huko unaitwa ‘Burudani’ ambao ni ugonjwa wa ngozi na unaambukiza, chanzo chake ni kunguni na chawa”. 
”Segerea kuna mahabusu kati ya 2300 mpaka 2450 lakini uwezo wa gereza hilo ni mahabusu 750, watu wanalala kitu kianaitwa ‘mchongoma’ yaani mnalala kwa ubavu mmoja kwa masaa matatu kisha mnageuka,” amesema Mbowe.

Mbowe ameshauri vyombo vya kutoa haki viweke mikakati ya namna ya kupunguza mahabusu, akidai kwamba vyombo hivyo kama vitapitia vizuri makosa ya mahabusu hao, itagundua kuwa nusu ya wafungwa walioko magerezani hawakustahili ... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More