Mbowe ajibu tuhuma za Mbunge aliyehama Chadema kwa madai alitelekezwa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbowe ajibu tuhuma za Mbunge aliyehama Chadema kwa madai alitelekezwa

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amekanusha taarifa zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa chama hicho katika jimbo la Ukerewe kuwa chama hicho kilimtelekeza wakati wa msiba wa ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere, akidai kuwa chama hicho kilimpatia rambirambi mbunge huyo.


Mbunge Joseph Mkundi aliandika barua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugai akieleza kujiuzulu uanachama wa CHADEMA, udiwani pamoja na ubunge wa jimbo lake kwa madai ya chama chake kukosa utu kwa kumtelekeza katika wakati wa majonzi.


Katika mahojiano yake na East Africa Breakfast kinachoruka kupitia East Africa Radio, Mbowe amesema maneno ya mbunge huyo katika barua ya kujiuzulu ni tofauti na taarifa aliyoitoa katika kipindi cha msiba ambapo alieleza kuwa chama chake kipo bega kwa bega na yeye.


“Imekuwa kawaida kwa kila anayehama anatoka na sababu zake za kitoto, kama yeye anasema hakupewa ushirikiano na wakati awali katika taarifa yake alisema anatambua mchango wa chama katika msiba ule lakini... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More