MBOWE , ESTER MATIKO 'MAMBO MAGUMU' , WARUDISHWA TENA MAHABUSU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBOWE , ESTER MATIKO 'MAMBO MAGUMU' , WARUDISHWA TENA MAHABUSU

Kuna kila dalili Sikukuu ya Krismass, Mwaka mpya wakasheherekea wakiwa ndani.
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
KESI ya tuhuma za uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko na wenzao saba inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Desemba 21 mwaka huu.
Aidha Mahakama hiyo imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuendelea kuhudhuria michezo ya Afrika Mashariki nchini Burundi na pia imeruhusu Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, kumuuguza mkewe ambaye amejifungua kwa upasuaji hivi karibuni.
Mbowe na Matiko wataendelea kukaa mahabusu kwa muda usiojulikana pengine hadi mwakani, baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.
Hatua hiyo imetokana na upande wa Serikali kukata rufaa kupinga uamuzi ya Jaji Sam Rumanyika aliyesema kuwa rufaa ya kina Mbowe ipo mahakamani hapo kisheria ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More