Mbunge apigia debe matumizi ya bangi - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbunge apigia debe matumizi ya bangi

Wakati Serikali hapa nchini ikipinga matumizi ya bangi, huku wanakamatwa nayo wakiishia mikononi mwa dola, Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM) ameishauri Serikali iruhusu matumizi ya bangi kwa kile alichodai kuwa mmea huo unatumika kutengenezea  dawa nyingi za maumivu.


Kishimba ametoa pendekezo hilo wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019, ambapo ameiomba wizara hiyo, kuchukua hatua za makusudi ili kuweza kuruhusu mmea huo ulimwe na wakulima hapa nchini.


“Sisi wenyewe tunayo bangi ukweli bangi hiyo sio kwa ajili ya kuvuta ni inaenda ,Lethoto na Zimbabwe wameruhusu. Gunia moja la bangi ni milioni 4 mpaka 5, bangi yote hii ya Tanzania inaenda katika madawa ya binadamu kuna ubaya gani Serikali itoe vibali ili watu walime bangi? Waziri wa Kilimo awasiliane na wa Afya kwani bangi hailiwi na wadudu ekari moja ya bangi unapata gunia sita” amesema Kishimba.


Hoja ya Kishimba imeonekana kumfurahisha Spika Jo... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More