Mbunge Ditopile atimiza ahadi aliyoitoa mbele ya Rais Magufuli - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbunge Ditopile atimiza ahadi aliyoitoa mbele ya Rais Magufuli

Charles James, Michuzi TV
Mbunge wa Viti Maalum Taifa anayewakilisha kundi la vijana, Mhe Mariam Ditopile ametimiza ahadi aliyoitoa mbele ya Rais Dk John Magufuli alipofanya ziara wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Mhe Ditopile aliahidi kuchangia mabati 200 yenye thamani ya Sh Milioni Tano kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Sagara ambayo iliezuliwa na upepo mkali na hivyo kusababisha changamoto kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Amesema yeye kama Mbunge anayewakilisha vijana ni lazima aoneshe kwa mfano utumishi wake kwa vijana ambao aliomba ridhaa ya kuwatumikia bila kujali itikadi zao.
" Nwapongeze waalimu kwa uzalendo wenu wakuendelea kuwafundisha watoto hawa katika mazingira haya magumu naamini Mwenyezi Mungu atawalipa hapa hapa Duniani na kesho kwa namna mnavyojitoa kwa kizazi hiki ambacho ndio Taifa la kesho.
" Niwafikishie salamu za Rais Magufuli anawasalimu sana wana Sagara na naamini atakuja mwenyewe kuja kujionea ukarabati huu, pia anasema anawapenda sana," amesema Mhe Ditopile.
Aidha Mhe Di... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More