MBUNGE GULAMALI AELEZWA NAMNA CHUO CHA NIT KILIVYOJIPANGA KUWAPOKEA WATALAAM WA BOEING ILI KUWANOA ATCL - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBUNGE GULAMALI AELEZWA NAMNA CHUO CHA NIT KILIVYOJIPANGA KUWAPOKEA WATALAAM WA BOEING ILI KUWANOA ATCL

Na Francis Daudi, Glogu ya jamii
MBUNGE wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali amtembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho kimejidhatiti kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Usafirishaji nchini Tanzania kwa kuzalisha wataalamu wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano katika kujenga Tanzania ya Viwanda. 
Akizungumza leo chuoni hapo baada ya kupokelewa na Mkuu wa chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa, Gulamali amesema amefurahishwa na utendaji kazi sambamba na mikakati iliyopangwa katika kuhakikisha sekta ya usafirishaji inakua zaidi.Amesema kuwa amefurahi kuona chuo alichosoma kinaendelea kuzalisha wataalamu zaidi katika sekta ya usafirishaji ambayo inachangia uchumi wa Taifa kwa asilimia kubwa.
Pia chuo hichokinaonesha jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli na amehaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali pindi itakapohitajika.
Akiwa Chuoni hapo Gulamali alipata fursa ya kutembelea Shule ya usafiri wa anga (School of Aviation) yenye madarasa ya waendesha ndege, karakana maalumu za kutengeneza injini za ndege na baadaye alitembelea idara ya ukaguzi wa magari na kueleza kufurahishwa na utendaji kazi unaofanywa kwa kutumia teknolojia ya juu. Mbunge wa Manonga Seif Gulamali ( kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo cha usafirishaji nchini (NIT) mara baada ya kumaliza ziara yake chuoni hapo. Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya vifaa katika karakana chuoni hapo kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa.Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akiwa katika chumba cha uongozaji wa ndege katika chuo cha usafirishaji (NIT) mara baada ya kufanya ziara  Chuoni hapo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>


Source: Issa MichuziRead More