Mbunge kutoka CCM ashindwa kufukuzana na ‘Speed’ ya Rais Magufuli, Akataa kugombea tena uchaguzi mkuu 2020 - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbunge kutoka CCM ashindwa kufukuzana na ‘Speed’ ya Rais Magufuli, Akataa kugombea tena uchaguzi mkuu 2020

Mbunge wa Rorya kwa tiketi ya CCM,  Lameck Airo, amesema kuwa hatogombea tena ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao 2020 na badala yake atawaachia vijana wapambanie nafasi hiyo.Mhe. Airo ambaye kwasasa yupo katika ziara jimboni mwake, amesema  tayari amewasilisha taarifa hiyo kwenye chama chake juu ya kusudio lake na kwamba wamekusudia kuwa mchakato wa uchaguzi utakapoanza, watahakikisha Jimbo la Rorya linaongozwa na vijana shupavu na wenye sifa.


Mbunge huyo ambaye amekuwa madarakani kwa mihula miwili, amesema atatimiza ahadi zake zote alizoahidi wakati wa kampeni za mwaka 2015 na kwamba kazi aliyofanya kwa miaka tisa, itabaki kuwa historia.


Kwa upande mwingine, Katika ziara hiyo pia alimkabidhi Diwani wa Kata ya Nyamtinga, Chacha Nyambaki (CCM) mabati 200, mifuko ya saruji 100 na Sh milioni moja kumalizia uezekaji wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule zilizoezuliwa paa kwa upepo.


Kama mbunge nitahakikisha kwa kipindi kilichobaki cha mwaka mmoja  kabla ya Uchaguzi Mkuu, ahad... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More