Mbunge Msukuma adai wasanii wanatumia michango ya misiba kujinufaisha - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbunge Msukuma adai wasanii wanatumia michango ya misiba kujinufaisha

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma, amesema kinachofanya hivi sasa tasnia ya sanaa hapa nchini kuporomoka ni kutokana na watanzania wengi wamekuwa si wafatiliaji wa kazi za wasanii wa ndani.


Msukuma ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma, wakati alipokuwa akichangia hoja  baada ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwasilisha makadirio na mapato ya matumizi ya wizara yake.


Katika hoja yake Msukuma amesema hivi sasa sanaa ya Tanzania, inakwenda kufa kwani angalau soko la muziki, kwa kuwa wanamuziki wengi hawategemei kuuza kazi zao isipokuwa wanafanya matamasha ya majukwaani, tofauti na sanaa ya filamu ambapo kwa sasa iko hoi.


Ameendelea kusema wasanii wengi wa filamu wamekuwa wakitegemea fedha za michango ya misiba kujinufaisha


“Tasnia ya filamu iko hoi bin taaban, ndo maana unakuta wasanii wetu wa bongo movie hawana kitu, sasa hivi wanategemea misiba, wapate michango na kufungua madanguro na kuwa makuwadi kwa wanaume,  wako hoi na hii ... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More