MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI WAWEKA TAA KIWANJA CHA MPIRA CHA KWALA KILIOPO MOMBASA KWA MCHINA UNGUJA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI WAWEKA TAA KIWANJA CHA MPIRA CHA KWALA KILIOPO MOMBASA KWA MCHINA UNGUJA.

Khadija Khamis – Maelezo  ZanzibarMbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Ibrahim Raza amesema ushirikiano wa wananchi na viongozi wa jimbo ndio hatua bora inayoleta ufanisi wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinatekelezwa kwa vitendo. Aliyasema hayo huko katika kiwanja cha mpira cha Kwala, Mombasa, wakati akizungumaza na waandishi wa habari walipofika kuangalia Taa zilizowekwa katika kiwanja hicho na kukiwezesha kutumika wakati wa usiku
Taa hizo zimewekwa kwa ajili ya kuwapa fursa vijana kucheza wakati wote na kukuza vipaji walivyanavyo na hatimae kupata nafasi ya usajili kwa vilabu vikubwa.  Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mahamoud Thabit Kombo alisema baada ya kiwanja hicho kuwekwa taa, wanampango wa kukiimarisha zaidi kwa kukiweka nyasi badia.
Alisema lengo ni kuimarisha michezo katika jimbo la Kiembesamaki ikiwa ni moja ya njia ya kutengeneza ajira kwa vijana na kuwaepusha na vitendo viovu. Aliwataka vijana wanaoishi karibu na kiwanja hicho kuwa wali... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More