Mbwana Samatta amemjibu Mbappe - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mbwana Samatta amemjibu Mbappe

Kinda wa Serengeti Boys Kelvin John ‘Mbappe’ kwa kinywa chake alitamka kwamba role model wake ni Mbwana Samatta, mtu ambaye anamfuatilia sana namna ya uchezaji wake na anatamani one day afikie level zake.


Salam hizo tukazifikisha kwa kwa mwenyewe Mbwana Samatta kwamba kuna dogo anatamani kuwa kama wewe na ikiwezekana avuke kwenda mbali zaidi.


Majibu ya Samatta yalikuwa hivi: “Nimefanya kazi kubwa kuwashawishi vijana wengine kucheza kwa kiwango ambacho mimi nimefika au kwenda mbali zaidi, kwa hiyo ni jambo kubwa na mimi nafurahi lakini nawausia kwamba wanaweza kuwa bora kuliko mimi si tu kufika ambako mimi nimefika lakini wanaweza kuvuka kwa hiyo waendelee kujituma nina imani watafanikiwa zaidi.”


“Niliongea nae (tulichati kwa kifupi) nilimweleza baadhi ya mambo kubwa ni juhudi halafu siku zote hakuna njia rahisi kufanikiwa. Inawezekana leo watu wakaona Samatta yupo sehemu fulani wakadhani ilikuwa rahisi alitoka akapambana akafika alipofika.”


“Hakuna njia rahisi ya mafaniki... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More