MBWATE WACHOSHWA NA KERO YA UKOSEFU WA MAJI NA UMEME - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MBWATE WACHOSHWA NA KERO YA UKOSEFU WA MAJI NA UMEME

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha WAKAZI wa mtaa wa Mbwate,kata ya Mkuza Kibaha Mjini mkoani Pwani, wanatatizo kubwa la ukosefu wa maji safi na salama ,hali inayosababisha kutumia maji ya kisima licha ya kuishi mjini. Aidha wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa nishati ya umeme ambapo tangu wawekewe nguzo ni takriban miezi nane bila muendelezo wowote.
Wakielezea kero zinazowakera ,akiwemo Kambangwa Kilema na Editha wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,kata ya Mkuza, walisema inashangaza kutumia maji yasiyo salama kwa kushirikiana na ngedere. Alisema ,wanataabika na hali hiyo licha ya serikali kuahidi kumtua ndoo mama kichwani. 
"Sijui tuko mjini ya wapi, hatupishani na wanaoishi kijijini, hatuna maji salama, hatuna umeme, tunaiomba serikali ituangalie kwa jicho la tatu ili nasi tufaidike na huduma hizi muhimu "alifafanua Kilema. Hata hivyo, Kilema aliweka bayana juu ya changamoto ya ukosefu wa umeme, na kudai wamekuwa wakienda shirika la umeme Tanesco kuomba wasaidiw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More