MC LUVANDA APANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU TUHUMA TATU - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MC LUVANDA APANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU TUHUMA TATUMtuhumiwa Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa amejifunika usoni leo jijini Dar es Salaam.
Na Karama Kenyunko,blogu ya Jamii.MSHEHERESHAJI maarufu nchini,Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda pamoja na kampuni yake,amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.
Luvanda anashtakiwa pia kwa kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mbali na luvanda washtakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo Leo Septemba 24 kwa makosa kama hayo mbele ya mahakimu watatu tofauti ni pamoja na Fadhili Kondo, Michael Mligwa na kampuni ya Luvanda ya Home of Company Limited.
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yanayowakabili mahakamani hapo kwa nyakati tofauti mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Hakimu Mkazi Mkuu, Hamza Wanjah 
Akimsomea mashtaka MC Luvanda, wakili ... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More