MC Luvanda Apewa ONYO na Mahakama - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MC Luvanda Apewa ONYO na Mahakama

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda kwa kusafiri bila ya ruhusa ya Mahakama.
Onyo hilo limetolewa leo Jumatatu Novemba 19, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi mbele ya mshtakiwa Luvanda, wakili wake Jebra Kambole na wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya wakili Kishenyi kuieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba mara ya mwisho kulikuwepo na amri ya Mahakama ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa kusafiri bila ruhusa ya Mahakama.
Wakili Kishenyi ameeleza Mahakama kwa sababu ametokea akumbushwe masharti ya dhamana.
Baada ya wakili Kishenyi kueleza hayo, wakili wa Luvanda, Jebra Kambole amedai yeye hana pingamizi kuhusu mshtakiwa kukumbushwa masharti ya dhamana na akaomba radhi kwa yaliyotokea na kwamba mambo hayo hayatajirudia tena.
Hakimu Shaidi alimwambia mshtakiwa huyo kila kitu kina nidhamu yake, pia hata katika kesi na kufika mahakam... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More