Mchawi Mweusi apigwa STOP JKT Tanzania - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mchawi Mweusi apigwa STOP JKT Tanzania

Katibu wa klabu ya JKT Tanzania Abdul Nyumba amethibitisha klabu yao kumsimamisha kwa muda kocha wao mkuu Bakari Shime Mchawi Mweusi kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya.


Nyumba amesema hawajavunja mkataba na Shime lakini kwa sasa hatohusika katika kuifundisha timu wala kukaa kwenye benchi la ufundi wakati wa mechi zao.


“Ieleweke kwamba hatujavunja mkataba wa kocha wetu mkuu, amesimamishwa kwa muda hadi tutakapotangaza uamuzi mwingine kumrudisha au kuachana naye. Kwa sasa hatofundisha timu.”


SOURCE: Azam TV


Source: Shaffih DaudaRead More