Mchezaji apoteza maisha kwenye ajali ya gari - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mchezaji apoteza maisha kwenye ajali ya gari

Kiungo wa klabu ya Free State ya nchini Afrika Kusini, Sinethemba Jantjies amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30.


Sinethemba amepata ajali ya gari wakati gari lake lilipogongana na gari lingine mapema hivi leo asubuhi.


Msimu huu Sinethemba alicheza michezo 23 na kufunga magoli 4 pamoja na kutengeneza goli moja.


Alianzia soka lake kunako klabu ya Mbombela, kabla hajajiunga na Free State.


Hata hivyo Sine alisaini mkataba wa awali na klabu ya Bidvest ambayo alipaswa kujiunga nayo mwezi julai mwaka huu.


Source: Shaffih DaudaRead More