Mchezaji Humoud aliyetimuliwa KMC kisa kutongoza wake wa wachazaji wenzake afunguka - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mchezaji Humoud aliyetimuliwa KMC kisa kutongoza wake wa wachazaji wenzake afunguka

Mchezaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga KMC Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’ (31) amesema klabu yake hiyo imemtengenezea shutuma.Gaucho ambaye aliipandisha daraja timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) alisema viongozi wa wa timu hiyo wanaongea maneno ambayo si ya kweli na walichopanga ni kumchafulia taswira yake bora ambayo imeitafuta kwa jasho zaidi ya miaka kumi.


Anasema mimi nilivunja mkataba na klabu ya KMC mwezi mmoja na nusu na kilichonifanya kuvunja ni kutokakana sikuwa napata nafasi ya kucheza bila ya sababu ya msingi tangu mwalimu mpya alivyofika.


“Niliandika barua ya kuomba kuachwa baada ya kushauriana na watu zangu wa karibu lakini nilipata majibu ambayo hayakuwa mazuri kutoka kwa viongozi wangu,” alisema.


“Majibu ambayo walinipatia natakiwa kurudisha vifaa vya timu na baada ya muda watakaa na wanasheria wao ili niwalipe ambavyo natakiwa kufanya hivyo jambo ambalo nalishangaa wakati mimi niliandika barua ya kuomba ambayo walikuwa na uwezo wa kunikatali... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More