MCHEZAJI MPYA RASTA AINUSURU YANGA KUPIGWA NYUMBANI NA NDANDA FC, WATOA SARE 1-1 UWANJA WA TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MCHEZAJI MPYA RASTA AINUSURU YANGA KUPIGWA NYUMBANI NA NDANDA FC, WATOA SARE 1-1 UWANJA WA TAIFA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
YANGA SC imepinguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Sare hiyo inaiongezea pointi moja Yanga SC ikicheza mechi ya 10 na kufikisha pointi 26, sawa na mabingwa watetezi, Simba SC waliocheza mechi 11 ambao wanaendelea kukamata nafasi ya pili kwa wastani wao mzuri wa mabao.   
Vigogo hao wote wapo nyuma ya Azam FC, yenye pointi 30 baada ya kucheza mechi 12 kufuatia na leo kupata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Mchezaji mpya, Jaffar Mohammed akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Yanga bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 na Ndanda FC

Katika mchezo wa leo, Ndanda walitangulia kupata bao mapema tu dakika ya 16 kupitia kwa Nassor Hashim aliyefumua shuti baada ya kupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji mwenzake wa Ndanda FC, Vitalis Mayanga aliyempindua beki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More