MCHEZAJI WA ALLIANCE ALIYEMTOMASA MAKALIO GARDIEL MICHAEL AFUNGIWA MECHI TATU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MCHEZAJI WA ALLIANCE ALIYEMTOMASA MAKALIO GARDIEL MICHAEL AFUNGIWA MECHI TATU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZAJI wa Alliance FC ya Mwanza, Juma Nyangi amefungiwa mechi tatu na faini ya Sh. Milioni 2 kwa kitendo cha kumtomasa makalio beki wa Yanga, Gardiel Michael.
Kipa Benedict Mlekwa Tinoco amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 14 2019 kati ya timu yake ya Mtibwa Sugar na Biashara United Fc alimkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu
Mlalamikiwa aliwakilishwa na kiongozi wa Timu yake, Ndg. Swabura Abubakar, mwakilishi wa mlalamikiwa alikiri kosa na kuomba msamaha.
Kamati imemtia hatiani Benedict Mlekwa Tinoco kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF ingawa ana Haki ya kukata rufaa.
Meneja wa  Transiti Camp, John Mchemba amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31,... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More