MECHI YA TAIFA STARS NA HARAMBEE YASOGEZA MBELE ‘SIKU YA MWANANCHI’ YANGA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MECHI YA TAIFA STARS NA HARAMBEE YASOGEZA MBELE ‘SIKU YA MWANANCHI’ YANGA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KILELE cha Siku ya Mwananchi, tamasha maalum la kutambulisha kikosi kipya cha Yanga SC lililopangwa kufanyika Julai 27, limesogezwa mbele.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dismass Ten katika mkutano wake na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam.
Ten amesema kwamba sababu za kusogezwa mbele kwa Siku ya Mwananchi ni kupisha mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2020 Cameroon kati ya Tanzania na Kenya.
Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Harambee Stars Julai 27 katika mchezo wa kwanza Raundi ya kwanza ya mchujo wa kuwania fainali za CHAN 2020, michuano inayoshusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kabla ya timu hizo kurudiana Agosti 2 mjini Nairobi.
Na kwa sababu hiyo, tarehe mpya ya kilele cha Siku ya Mwananchi itatangazwa upya, lakini tayari kikosi cha Yanga SC kipo kambini mjini Morogoro chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Msambia Noel Mwandila kikijiandaa na msimu mpya. ... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More