MELI YAUNGUA MOTO BAGAMOYO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MELI YAUNGUA MOTO BAGAMOYO


NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
Meli kubwa ya mizigo iitwayo MV RAHIMA (LAND CRAFT RAHIMA) imeungua moto kwa asilimia 20,katika bandari ya Bagamoyo,mkoani Pwani.

Meli hiyo inayomilikiwa na Hamis Rashid mkazi wa Unguja ilikuwa ikiongozwa na kapteni Abdulrahman Abdulaziz ambae ni mkazi wa Unguja na ina uwezo wa kubeba mzigo wenye ukubwa wa tani 500 kwa mara moja.MV RAHIMA imekaa kwa muda wa wiki moja katika bandari ya Bagamoyo ikisubiri kupakia mzigo wa mifuko ya saruji wa tani 300 na ndani ya meli kulikua na watu 16 ambao ni mabaharia na wafanyakazi wengine wa meli.

Akielezea chanzo cha moto huo ,kapteni wa meli hiyo Abdulrahman Abdulaziz alisema ni hitilafu ya umeme .“Mlango wa mbele wa meli ulikua umeharibika, hivyo alfajiri ya tarehe 14 agosti, tuliamkia kuutengeneza kwa kuuchomelea maana ulikua na hitilafu, tayari kwa kujiandaa kupokea mzigo na kuanza safari ya kurudi Unguja”alisema Abdulrahman.

Alielezea, wakiwa katika kutengeneza mlango huo, ghafla waliona moshi mkubwa en... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More