Meneja Simba afungiwa ndani na nje - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Meneja Simba afungiwa ndani na nje

Kamati ya maadili ya TFF imemfungia meneja wa klabu ya Simba Richard Robert kutojihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni 4 baada ya kumkuta na hatia ya kuihujumu timu ya taifa na kutotii maagizo ya TFF.


Adhabu ya kuhujumu ni kwa mujibu wa kifungu 5 (2), kifungu cha 6(c) na (h) vya kanuni za maadili za TFF toleo la 2013 na adhabu ya kutotii maagizo ya TFF ni kwa mujibu wa kifungu cha 41 (8) cha kanuni za ligi kuu toleo la 2013.


“Team manager yeye ndio anakaa na wachezaji pamoja na kocha, ndio mtu wa katikati kati ya utawala mwalimu. Anasema alipoambiwa akamwambia kocha mkuu, kocha akasema hapana hadi achunguze ukweli wa hilo jambo uko vipi”-Hamidu Mbwezeleni, Mwenyekiti kamati ya maadili TFF.


Source: Shaffih DaudaRead More