MENEJA WA SIMBA SC AFUNGIWA MWAKA NA FAINI MILIONI 4 AKIDAIWA KUSABABISHA AKINA KICHUYA WASIINGIE KAMBINI STARS - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MENEJA WA SIMBA SC AFUNGIWA MWAKA NA FAINI MILIONI 4 AKIDAIWA KUSABABISHA AKINA KICHUYA WASIINGIE KAMBINI STARS

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) imemfungia Meneja wa Simba SC, Richard Robert kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. Milioni 4.
Hiyo ni baada ya Kamati hiyo chini ya Mwanyekiti wake, Hamidu Mbwezeleni kumkuta na makosa mawili ya kuihujumu timu ya taifa na kushindwa kutii agizo la TFF – lakini atatumikia kifungo cha miezi sita kutokana na adhabu zake kwenda sambamba. 
Mbwezeleni amesema katika mkutano na Waandishi wa Habari leo kwamba adhabu ya kuhujumu ni kwa mujibu wa kifungu 5 (2), kifungu cha 6 (c) na (h) vya Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013 na adhabu ya kutotii maagizo ya TFF ni kwa mujibu wa kifungu cha 41 (8) cha kanuni za ligi kuu toleo la 2013.

Meneja wa Simba SC, Richard Robert (kushoto) amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka 

Robert anadaiwa kuwa sababu ya wachezaji wa Simba SC, mabeki Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, viungo Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Shiza Kichuya na mshambuliaji John Bocco wa Simba... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More