Messi amwagia Ronaldo sifa, asema Atletico imemchania mkeka - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Messi amwagia Ronaldo sifa, asema Atletico imemchania mkeka

Kumekuwa na picha inasambaa mtandaoni ikionesha mawasiliano ya whatsapp kati ya Evra na Ronaldo. Katika mazungumzo hayo Evra anamsihi Ronaldo kuhakikisha kuwa anawatoa Atletico.


“Bro kila unaposhindwa kufunga au Juve ikifungwa nakosa amani mtaani. Kila mtu ananizomea. Nakuaminia kaka” Evra


Ronaldo akamjibu akamwambia “Usijali bro”


Sasa baada ya Ronaldo kutimiza ahadi ya Evra, Messi amejitokeza na kumwagia sifa kedekede mchezaji huyu bora kabisa kuwahi kutokea katika michuano ya UEFA kwa kudai kuwa alifanya maajabu.


“Nilitegemea sana Atletico wataleta ubishi kutokana na uimara wao wa kuzuia. Lakini Ronaldo alifanya miujiza.”


“Sikutarajia kama Juventus wangepita, hongera kwa Ronaldo kwa kufunga magoli mawili” Messi.


#Class #Legend #MessiRonaldo


Source: Shaffih DaudaRead More