Mfahamu fundi aliyetengeneza gereji inayotembea, Tunduma wanamuita ‘Street Engineer’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mfahamu fundi aliyetengeneza gereji inayotembea, Tunduma wanamuita ‘Street Engineer’

Adam Zakaria Kinyekire anajulikana zaidi kwa jina la ‘Street Engineer’, yeye ni fundi mekanika kutoka Wilaya ya Tunduma, Mkoa wa Songwe, nyanda za juu kusini mwa Tanzania.


Adam amewasaidia vijana wengi kwa ajira


Alijifunza kazi hiyo mwenyewe bila kuhudhuria chuo chochote, lakini ni maarufu kwa kuunda helikopta na pia huwafaa madereva kwa gereji inayotembea.


Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Adam anasema yeye ni mbunifu ambaye hakupata ujuzi wowote kutoka shuleni maana mara baada ya kumaliza shule ya msingi, alianza kujifunza kutengeneza magari katika karakana ya kawaida na baadaye akaanza kuunda vitu kama vile mashine ya kusagia nafaka, gari la karakana na hata helikopta.


Gereji


“Ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali huwa sifundishwi na mtu ni kitu tu ambacho kipo kwenye damu, ni kama vile ndoto tu ambapo vitu vinakuja kwenye akili kwamba naweza kutengeneza hiki na hiki lakini sijawahi kupata mafunzo popote,” Adam Zakaria anaeleza.


Kwa sasa anafanya kazi na vijana takribani 40 na wengine zaidi ya 500 walipita katik... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More