Mfahamu kiundani Rais mpya wa DR Congo, Felix Tshisekedi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mfahamu kiundani Rais mpya wa DR Congo, Felix Tshisekedi

Felix Tshisekedi ni mtoto wa aliyekuwa kiongozi mahiri wa upinzani Etienne Tshisekedi aliyefariki dunia hivi karibuni. Je mtoto huyo anacho kifua cha kutuliza ghasia katika nchi yenye wakaazi Milioni 80?. Akizungumza na waandishi habari siku ya Alhamis(10.01.2019) Felix Tshisekedi alisema, “hakuna aliyeweza kuwaza kwamba ushindi wa,mgombea wa upande wa upinzani ungeliweza kuthibitika.” Tshisekedi amesema wapiga kura wametamka ukweli na ameahidi kuwa rais wa wote katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Mwanasiasa huyo alizaliwa mjini Kinshasa mnamo mwaka 1963. Ana mke na watoto watano. Baba yake Etienne alijaribu kuwapa changamoto marais watatu lakini hakufanikiwa, bila ya mafanikio. Mara ya mwisho baba Etienne alishindwa na rais Joseph Kabila kwa madai kwamba aliibiwa kura.

Kwa mujibu wa DW Swahili, Harakati za akina Tshisekedi dhidi ya udikteta nchini Congo zilianza mnamo mwaka1982. EtienneTshisekedi alianzisha chama cha kidemokrasia na maendeleo ya kijamii katika mji... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More