MFAHAMU MICHAEL KEARNEY KIJANA ALIYEMALIZA CHUO AKIWA NA MIAKA 10 PEKEE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFAHAMU MICHAEL KEARNEY KIJANA ALIYEMALIZA CHUO AKIWA NA MIAKA 10 PEKEEMICHAEL Kearney raia wa Marekani ndiye kijana pekee aliyevunja rekodi ya kumaliza chuo akiwa na umri mdogo kabisaa wa miaka 10 na kuwa mwalimu wa chuo kikuu akiwa bado kijana.
Michael alizaliwa Januari 18, 1984 familia yake ikinukuliwa na jarida la Chuo cha San Marin ilieleza kuwa Michael alianza kufundishwa na wazazi wake kabla ya kwenda shule na hiyo ni baada ya kuona namna anavyokuwa na kichwa chepesi na akili zilizopitiliza katika kuelewa mambo, imeelezwa kuwa hata dada yake Michael aitwaye Maeghan alimaliza chuo akiwa na miaka 16 pekee.
Imeelezwa kuwa akiwa na miezi minne pekee Michael alitamka neno la kwanza na akiwa na miezi 10 alijifunza kusoma na alipofika miaka 4 alifahamu na kujua hesabu akiwa hajaanza shule kabisa.
Akiwa na umri wa miaka 6 alienda shule ya San Marin kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kijiunga na elimu ya juu.
Akiwa na miaka 10 Michael alipata shahada yake ya kwanza katika fani ya Anthropolojia, na alipofika miaka 14 alipata shahada ya uzamili katika chuo cha ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More