MFANYABIASHARA AFIKISHWA KORTIN KWA KUDAIWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFANYABIASHARA AFIKISHWA KORTIN KWA KUDAIWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

Na Karama Kenyunko globu ya jamii.
MFANYABIASHARA Andres Uribe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la  kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine Hydrochloride.
Uribe amefikishwa mahakamani hapo leo Juni 17,2019 ambapo amesomewa shtaka lake tmbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Mmbando.
 Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda amedai kuwa Agosti 11, 2014 katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA), mshtakiww alisafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 904.7 ambayo yana thamani ya Sh milioni 63.3.
Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.
Kwa mijibu wa upande wa mashitaka,  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na  kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai Mosi, mwaka huu kwa kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande. MFANYABIASHARA Andres Uribe alipofikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo  akikabiliwa na... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More