MFANYABIASHARA DAR AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKWEPA KODI, KUJIPATIA BILIONI 188.9/- - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFANYABIASHARA DAR AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKWEPA KODI, KUJIPATIA BILIONI 188.9/-

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MFANYABIASHARA Mustapha Kambangwa (34) ambaye ni Mkazi wa Kongowe Mbagala, jijini Dar es Salaam amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kukwepa kodi na kujipatia Sh.bilioni 188.9 kupitia mashine ya kieletroniki (EFD).
Mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtenga imedaiwa na Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa kuwa katika siku tofauti kati ya Juni Mosi ,2016 na Novemba 2, 2018 mshitaka Kambangwa alijifanya kama mtu aliyesajiliwa kuwa mlipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kukusanya kodi ya VAT  Sh.188,928,752,166 kwa kujifanya anakusanya fedha hizo kwa niaba ya TRA.
Katika shtaka la pili, Msigwa amedai kati ya Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka huu, mshtakiwa kwa udanganyifu alitumia mashine ya kieletroniki (EFD) yenye namba 03TZ842011315 iliyosajiliwa kwa jina la Kampuni ya Abraham's Group LTD kukwepa kodi ya VAT yenye thamani kiasi hicho cha fedha.
Aidha ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More