MFANYABIASHARA KUJENGA MADRASA KASENYI SENGEREMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFANYABIASHARA KUJENGA MADRASA KASENYI SENGEREMA


NA BALTAZAR MASHAKA, SENGEREMA.
MKURUGENZI wa kampuni ya Baraka Mining inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu, almasi na vito, Baraka Chilu ameahidi kujenga madrasa itakayotumika kufundishia elimu ya dini hiyo, kununua pikipiki na mazuria ya msikitini hapo Kijiji cha Kasenyi wilayani Sengerema.
Pia Chilu ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri ya BAKWATA Sengerema alitoa fedha sh. 500,000 za kulipa posho ya miezi miwili ya mwalimu wa dini ya kiislamu, kati ya fedha hizo kiasi cha sh. 150,000 zitatumika kununulia baiskeli ya kumrahisishia usafiri wa kwenda na kurudi kutoa elimu kwenye shule za msingi na sekondari za Nyamahona.
Mgeni rasmi huyo wa maonyesho ya umahiri wa kuhifadhi Kuran na hadithi za Mtume Muhammad S.A.W.lililofanywa na wanafunzi wa madrasa ya Msikiti wa Kasenyi, alilionyeshwa kuguswa na changamoto ya wanafunzi hao kukosa sehemu sahihi ya kujifunzia elimu ya dini kutokan na risala iliyosomwa na katibu wa madrasa hiyo.
"Fanyeni tathmini ya gharama za ujenzi wa madrasa na ni... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More