MFANYABIASHARA MAARUFU NA MFANYAKAZI WAKE WASOMEWA MASHTAKA 601,LIKIWEMO LA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA ZAIDI YA BILIONI 14 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFANYABIASHARA MAARUFU NA MFANYAKAZI WAKE WASOMEWA MASHTAKA 601,LIKIWEMO LA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA ZAIDI YA BILIONI 14

Mfanyabiashara maarufu Mohamed yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 601 likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 14.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili wa kutoka Takukuru wakiongozwa na Hashimu Ngole, Pendo Makondo, Leornad Swai ambao walikuwa wakisaidiana na wakili wa serikali Patrick Mwita mbele ya hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika mashtaka hayo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa TRA, kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58

Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la kusabisha hasara ambayo imetokana na kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More