MFUKO WA KILIMO WA PAMOJA MBIONI KUANZISHWA KWA NCHI ZA SADC - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFUKO WA KILIMO WA PAMOJA MBIONI KUANZISHWA KWA NCHI ZA SADC

JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) imesema ipo kwenye mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa kanda kwa ajili ya kusaidia nchi wanachama wa jumuiya hiyo. 
Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2019 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa jumuiya hiyo Domingos Gove wakati anazungumza na waandishi wa habari za mikutano ya SADC inayoendelea jijini. 
“Kwa sasa tupo katika mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ambao lengo ni kuhakikisha tunasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC,” amesema Gove. 
Amefafanua katika mkakati huo pia watahakikisha kunakuwa na miundombinu itakayofanikisha nchi wanachama zinajikita kwenye kilimo kwa ajili ya kupata chakula cha kutosha kwa nchi zao. 
Mkurugenzi huyo wa Kilimo,Chakula na Maliasili ameongeza kuwa kwenye mfuko huo ambao utaanzishwa kwa nchi za SADC utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala la ki... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More