Mfumo wa upigaji kura wa kieletroniki wawacharua wapinzani DRC watishia kuandamana kupinga mfumo huo - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mfumo wa upigaji kura wa kieletroniki wawacharua wapinzani DRC watishia kuandamana kupinga mfumo huo

Wagombea wakuu wa upinzani kwa nafasi ya urais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, upinzani umeitisha maandamano ya kupinga mfumo wa kura kwa mashine za elekroniki kwenye uchaguzi mkuu wa Desemba 23. Upinzani unasema kuwa wanapinga pia daftari la wapigakura wasio na alama za vidole kwenye kadi zao. Hata hivyo, Martin Fayulu, mmoja wa wagombea wa urais na ambaye alisoma taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani mbele ya waandishi wa habari mjini Kinshasa, alisema upinzani hauna nia ya kuususia uchaguzi huo.“Tunawatolea wito raia wa Kongo kujipanga kwa ajili ya kulazimisha kuweko na kura ya makaratasi kulingana na sheria ya uchaguzi na kalenda iliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi.”


Licha ya hayo, wapinzani walisema wanaunga mkono juhudi zozote za mazungumzo ili kupata suluhisho kuhusu mfumo wa uchaguzi wa matumizi ya mashine ya elekroniki.


Taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani iliidhinishwa na Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Jean-Pierre Bemba, Moise Katumbi, Freddy Matungulu na Ma... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More