MFUMO WA USAMBAZAJI MAJI WA BAGAMOYO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA KUBWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MFUMO WA USAMBAZAJI MAJI WA BAGAMOYO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA KUBWA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamesema  kazi ya   ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji Bagamoyo imekamilika kwa asilimia kubwa maji yamefunguliwa na kufika katika tenki la Bagamoyo. Kazi ya usafishaji wa mabomba inaendelea kwa ufanisi  na inatarajiwa kukamilika  leo chini ya usimamizi Mhandisi  Lydia Ndibalema Mkurugenzi wa miradi wa Dawasa.na utakapokamilika maji yataanza kwenda tenki la maji la Bagamoyo linalohifadhi Lita Milioni sita kwa siku.
Mradi huo wa  Uliojengwa kwa mkopo wa  masharti nafuu na unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Desemba mwaka huu na wananchi wa mji wa Bagamoyo watafanikiwa kupata maji. Zoezi hilo la kusafisha mabomba  mji wa Bagamoyo utaanza kupata maji  kwa wingi na  kwa msukumo mzuri kupitia mfumo wa zamani, Mkandarasi wa kujenga na kupanua mfumo mpya wa usambazaji maji anatarajiwa  kupatikana wakati wowote.
Mradi huo Oktoba 25 mwaka huu ulitembelewa na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungan... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More