Mfumuko wa bei wapungua hadi kufikia asilimia 3.6 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mfumuko wa bei wapungua hadi kufikia asilimia 3.6

Na Chalila Kibuda, Globu ya JamiiMFUMUKO  wa bei wa Taifa  wa Mei 2018  umepungua  hadi kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na asilimia 3.8 ilivyokuwa Mwezi Aprili 2018 mwaka huu .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa bei kumechangiwa sana na kupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula.
Amesema  baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mahindi kwa asilimia 10.3, unga wa mahindi kwa asilimia 12.5, mtama kwa asilimia 13.8, unga wa mihogo kwa asilimia 15.2, viazi mviringo kwa asilimia 9.0 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.6, alisema bwana Kwesigabo.
Ameongeza kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2018.
Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More